AfyaHabari

RAIS UHURU KENYATTA ALIONGOZA TAIFA KATIKA MAADHIMISHO YA 18 YA MAOMBI YA KITAIFA……….

Rais Uhuru Kenyatta analiongoza taifa katika maadhimisho ya 18 ya maombi ya kitaifa yanayoendelea katika majengo ya bunge la Kitaifa.

Naibu wa rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi ambao wanahudhuria, wengine ni Jaji Mkuu Martha Koome, spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi, spika wa bunge la seneti Ken Lusaka, kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi, kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka, wabunge na viongozi wa kidini.

Seneta wa Busia Amos Wako amepewa nafasi ya kuhadithia mafunzo aliyopata kutokana na ugonjwa wa Covid 19. Wako amewahimiza wakenya kutopuuza dalili zinazohusiana na Covid 19 na kuwata kupimwa mara moja

Aidha Seneta Wako ameipongeza serikali ya kitaifa na Wizara ya Afya kwa juhudi kubwa ambazo wamefanya ili kukabiliana na janga la Corona nchini.

Wako hata hivyo ameirai serikali kuhakikisha kuwa maskini wanaweza kupata huduma za matibabu haswa katika matibabu ya COVID-19.

BY GLADYS MARURA