HabariSiasa

Mkutano wa Chama cha UDA watibuliwa mjini Mombasa……………………

Maafisa wa polisi hapa Mombasa wametibua kikao kilichoitishwa na maafisa wa chama cha UDA kinachohusishwa na naibu rais William Ruto kilichokuwa kinaandaliwa katika hoteli moja hapa mjini.

Polisi hao waliojihami kwa silaha wamevamia hoteli hiyo na kuwafurusha wafuasi wa chama hicho kwa madai ya kutekeleza sheria za kukabiliana na corona.

Wanahabari walikuwa wanafuatilia kikao hicho pia wamefurushwa na polisi hao.

Hata hivyo huenda hatua hii ikatajwa kuwa ni ya kisiasa kwani maafisa hao tayari walikuwa na idhini ya kuandaa mkutano huo.

 

By Warda Ahmed