Habari

OCS afikishwa mahakamani mjini Garissa……………….

OCS wa kituo cha polisi cha Garissa Michael Munyalo ambaye alifikishwa mahakamani hii leo ili kujibu mashtaka ya mauaji dhidi yake, ameachaliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 1.

Akitoa uamuzi wake kupitia mtandao wa Zoom, jaji wa mahakama hiyo ya garissa Abida Haruni ameamuru mshukiwa kupewa dhamana ya shilingi milioni 1 na mdhamini wa kiasi sawa na hicho.

Munyalo anadaiwa kumuua Moris Kimathi kwa kumpiga risasi sehemu nyeti baada ya wawili hao kutofautiana katika jumba moja la burudani tarehe 16 mwezi uliopita, mashtaka ambayo ameyakanusha.

Kesi hiyo itasikizwa tena tarehe 7 mwezi ujao

By Joyce Mwendwa