Habari

Haki Afrika kuwashtaki wanaowaachiliwa washukiwa wa dhulma za kijinsia…..

Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika limetishia kuwashtaki maafisa wa polisi wanaowaachilia huru washukiwa wa dhulma za kijinisia.

Afisa wa shirika hilo kaunti ya Kwale Abdulrahman Mwangoka amewataka wakuu wa idara ya polisi kufuatilia suala hilo ili maafisa hao wakabiliwe kisheria.

Mwangoka ameshtumu vikali hulka ya maafisa wa polisi ya kuwaachilia huru washukiwa wanaotekeleza visa vya dhulma katika jamii.

Kwa upande wake naibu kamishena wa eneo bunge la Lungalunga Hussein Alasu ameahidi kushirikiana na shirika hilo ili kuzuia ongezeko la visa hivyo.

Alasu amesisitiza kwamba polisi hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria washukiwa wa dhulma hizo.

 

By Kwale Correspondent