Habari

Mwanafunzi mmoja aaga dunia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani…………

Mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza katika shule ya upili ya wasichana ya Murray eneo  bunge la Mwatate kaunti ya Taita Taveta amedhibitishwa kuaga dunia baada ya matatu walimokuwa wakisafiria kuanguka katika mbuga ya wanyamapri ya Tsavo magharibi jana jioni.

Akithibitisha ajali hio, kamanda wa polisi eneo la Taveta Charles Baraza anasema ajali hiyo imetokea wakati dereva wa matatu hiyo iliyokuwa imewabeba wanafunzi waliokuwa wakirudi shuleni baada ya likizo fupi kuhepa kugonga ndovu kabla ya kubingiria katika barabara ya Taveta-Voi.

Baraza amesema kwamba mwanafunzi huyo wa alifariki wakati akikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kupata matibabu huku wenzake watatu wakipata majeraha mabaya ambapo wamesafirishwa hadi hapa Mombasa kwa matibabu zaidi .

Kulingana na afisa huyo matatu hiyo ilikua imebeba wanafunzi 13  huku tisa wakitibiwa katika hospitali ya mpakani ya Taveta na kuruhusiwa kuenda nyumbani.