Uncategorized

Wizara ya elimu yazindua masomo ya mazoezi na michezo kwa shule za umma…….

Waziri wa elimu proffesa George Magoha amezindua rasmi sera ya masomo ya mazoezi na michezo katika shule zote za umma, sera hiyo inafanya kuwa lazima kwa shule zote kuwa na masomo hayo rasmi.

Japo shule zina masomo hayo na hayatiliwi maanani na hayana mitihani, hali ambayo imemfanya waziri Magoha kuanza mchakato wa kuhakikisha kwamba mazoezi shuleni na michezo pia inafanyika kwa lazima, huku akiwataka walimu wakuu kuhakikisha kuna viwanja vya kutosha na kuregesha vile vilivyonyakuliwa.

 

By Warda Ahmed