Habari

Safaricom yapata leseni ya kuhudumu nchini Ethiopia……

Rais Uhuru Kenyatta amewaarifu wakaazi wa Ethiopia kutarajia manufaa makubwa kutokana na huduma za kampuni ya Safaricom iliyopata leseni ya kuhudumu katika taifa hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa rasmi leseni hiyo, rais KENYATTA ametumia mfano wa mchango mkubwa wa kampuni hiyo katika uchumi wa taifa kuwa kielelezo cha uwezo wake wa kuwanufaisha kwa njia mbali mbali raia milioni 112 wa Ethiopia.

Kampuni ya Safaricom ikishirikiana na kampuni nyingine kutoka Afrika Kusini,Uingereza na Japan ilishinda zabuni ya shilingi bilioni 91.8 ili kuanza huduma mbali mbali za mawasiliano.

Kwa mujibu wa zabuni hiyo shughuli zitaanza rasmi mwaka ujao.

Katika hotuba yake, rais ametaja uvumbuzi kama wa MPESA na mifumo mengine kurahisisha upatikanaji wa fedha miongoni mwa raia kuwa mchango mkubwa katika uchumi wa taifa.

Kwa upAnde wake waziri mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed ameelezea matumaini kwamba itafikia ufanisi sana kama ilivyofikia nchini Kenya.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na afisaa mkuu mtendaji wa safaricom Peter Ndegwa, Afisaa mkuu wa Vodafon nchini Afrika Kusini na mkuu wa mawasiliano nchini Ethiopia.

By Warda Ahmed