HabariNewsSiasa

Charity Ngilu awataka Raila na Kalonzo kuungana………..

Gavana wa Kitui Charity Ngilu sasa anasema kwamba iwapo kinara wa chama cha WIPER Kalonzo Musyoka hataungana na kinara wa ODM Raila Odinga katika uchaguzi mkuu ujao, basi naibu rais William Ruto ataibuka mshindi na kuwa rais kwa wepesi mno.

Akihutubu katika hafla ya mazishi ya Kalembe Ndile, Ngilu amesema yuko tayari kuwaunganisha wawili hao kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Hata hivyo gavana wa Machakos dkt Alfred Mutua amepinga vikali kauli ya Ngilu, akisema watamuunga mkono Kalonzo iwapo atadhihirisha uwezo wake wa kutwaa urais.

Majibizano haya yanajiri wakati ambapo Kalonzo tayari ameungana na viongozi kama vile Gideon Moi wa Kanu, Musalia Mudavadi wa ANC na Moses Wetangula wa Ford Kenya na kubuni muungano wa One Kenya Alliance OKA japo inasemekana kuna msukosuko na kutoelewana ndani ya muungano huo kuhusu nani anafaa kuwania urais.

By Warda Ahmed