HabariNews

Serikali kutumia shilingi bilioni 1 katika mradi wa maji Tanariver……..

Waakazi wa TanaRiver wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali kutumia shilingi bilioni 1 katika miradi ya maji kaunti hiyo.

Akizungumza katika ziara yake kaunti hiyo, katibu katika wizara ya maji Joseph Irungu amesema kuwa wizara ya maji ina miradi mingi eneo la Tana River mojawapo ikiwa wa kuchimbwa kwa visima vya maji katika kila kijiji.

Aidha amesema kuwa atashirikiana na viongozi wa kaunti hiyo kuhakikisha uhaba wa maji unatatuliwa, kwani serikali inanuia kuchimba visima zaidi ya mia kaunti hiyo.

Irungu aidha ameongeza kuwa wizara ya maji pia itachimba mabwawa ya maji ili kuwasaidia wafugaji kuhifadhi maji wakti wa msimu wa mvua.

By Joyce Mwendwa