Habari

GAVANA WA NAKURU LEE KINYANJUI KUHOJIWA NA KAMATI YA BUNGE YA LEBA

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui na mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI wanatarajiwa kuhojiwa na kamati ya bunge ya Leba na masuala ya kijamii hivi karibuni kufuatia kupotea kwa watoto watano wa kurandaranda mitaani.

Kamati hiyo imewaagiza wawili hao kufika mbele yake kueleza waliko watoto hao

Inasemekana watoto hao walikuwa miongoni mwa 41 waliohamishwa kwa lazima kutoka katikati ya mji wa Nakuru mwezi Februari mwaka 2019 na kutupwa katika msitu wa Chemasusu ulioko kwenye kaunti ya Baringo

seneta wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja amesema kamati hiyo pia italenga kufahamu mikakati ambayo kaunti ya Nakuru imeweka ili kuzitafutia makao mbadala familia za kurandaranda mitaani huku DCI ikitakiwa kueleza ilipofika katika uchunguzi wake kuwahusu watoto hao waliopotea.

 

BY JOYCE MWENDWA