AfyaHabari

MAKAFANI YA HOSPITALI YA RUFAA KAUNTI YA KILIFI KUFUNGULIWA MWEZI HUU

Serikali ya kaunti ya Kilifi imeshikilia msimamo wake kuwa makafani katika hospitali ya rufaa kaunti hiyo itafunguliwa mwezi huu wa Juni.

Kulingana na waziri wa afya kaunti hiyo Charles Dadu ni kuwa marekebisho madogo madogo ndiyo yanayoendelea kukamilika huku mipango yote ikiwa imekamilika kufikia sasa.

Kwa upande wao wahudumu  wa magari ya kubeba maiti wanasema tangu kufungwa kwa makafani hiyo biashara zao zimesambaratika.

Wahudumu hao wakiongozwa na Fedson Karisa wanasema wamekuwa wakitengemea kufanya kazi katika hifadhi za kibinafsi  ambapo hifadhi hizo ziko na magari yao ya kubebea maiti.

Ikumbukwe makafani katika hospitali ya rufaa kaunti ya Kilifi yalitarajiwa kufungwa kwa wiki mbili pekee kabla kufunguliwa rasmi, ila kufikia sasa ni takriban miezi miwili na nusu bado makafani hiyo haijafunguliwa.

 

BY ERICKSON KADZEHA