Habari

MFANYIBISHARA MASHUHURI NCHINI CHRISS KIRUBI AFARIKI DUNIA.

Mfanyibishara mashuhuri nchini Chriss Kirubi ameaga dunia.

Kulingana ana familia yake,Kirubi ameaga dunia akiwa na miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na maradhi ya saratani.

Mfanyibiashara huyo aliyekuwa anamiliki kampuni duka la Jumla la Two Rivers jijini Nairobi, Kituo cha radio cha Capital fm, Haco industries, DhL na zenginezo.

Tayari viongozi mbalimbali wakiongozwa na rais Uhuru Kenyatta, naibu wa rais William Ruto na kinawa wa ODM Raila Odinga wametuma salamu zao za rambirambi,akiwemo naibu wa rais William Ruto.

Katika ujumbe wake wa faraja, Rais Kenyatta amemtaja  Kirubi, 80, kama mfanyabiashara mwenye msimu, mjasiriamali na viwanda wa viwanda ambao walianzisha na kwa mafanikio waliendesha baadhi ya mashirika makubwa ya Kenya.

Kirubi aliorodheshwa na jarida la Forbes kuwa Mkenya wa pili kwa utajiri mwaka 2011 katika orodha iliyojumuisha familia ya kiongozi mwanzilishi wa nchi hiyo, Marehemu Rais Jomo Kenyatta.

Alifanikiwa pia kushika nafasi ya 40 ya tajiri zaidi barani Afrika baada ya katika nafasi ya 31, mali yake ikiwa na thamani ya dola milioni 300.

Bw. Kirubi atakumbukwa kwa kuwahimiza vijana kujiamini wanaweza bila kujali walikotoka akiongeza kwamba yeye pia alinzia chini na kufikia upeo wa maisha yake, baada ya kufiliwa na wazazi wake akiwa na umri mdogo.

By Hajj Kibwanga