Habari

Wakaazi Wasini Kwale wapinga unyakuzi wa ardhi yao….

Wakaazi wa kisiwa cha Wasini eneo la Lungalunga kaunti ya Kwale, wanapinga kile wanachodai ni unyakuzi wa ardhi ya ekari 289 katika eneo hilo.

Ardhi hiyo inadaiwa kunyakuliwa na bwenyenye mmoja anayedai umiliki wa kisiwa hicho.

Wakaazi hao wanadai kwamba vitengo vya serikali vinatumika vibaya kuwanyanyasa kwa lengo la kuwafurusha kutoka ardhi yao

Hata hivyo familia 89 ziko kwenye hatari ya kufurushwa kutoka eneo hilo, kwani tayari bwenyenye huyo amechapisha tangazo la uuzaji wa kisiwa hicho, kwenye jarida moja nchini kwa kima cha shilingi billion 1.3.

Wakaazi hao aidha wameshangazwa na madai ya umiliki huo licha ya kwamba wanamiliki hatimiliki za ardhi walizopewa na serikali katika miaka ya themanini.

 

.By Joyce Mwendwa