AfyaHabari

Wananchi Mombasa wahimizwa kutoa damu kila mwaka…..

Wananchi kaunti ya Mombasa wametakiwa kujitokeza na kutoa damu kila mwaka ili kuokoa maisha ya wagonjwa wengi ambao wanahitaji damu, baada ya kubainika kwamba kuna uhaba mkubwa wa damu katika kituo cha kuhifadhi damu nchini.

Kulingana na mwenyekiti wa bodi ya shirika la msalaba mwekundu kaunti ya Mombasa Mahmoud Noor, angalau wananchi elfu 14 wa kaunti ya Mombasa wanahitajika kutoa damu kila mwaka kulingana na kiwango kinachohitajika cha idadi ya watu.

Wakati huo huo amesema wao wakishirikiana na serikali wanaweka mikakati ili kuhakikisha hakuna ufisadi unaoshuhudiwa katika suala zima za hifadhi ya damu, huku akisema kwamba malipo wanayotozwa wananchi wanaopohitaji damu ni ya kufanyia vipimo damu hiy haswa katika hospitali za kibinafsi.

Zaidi ya wakenya milioni moja wanahitaji damu nchini wakiwemo kina mama waliojifungua na hata wagonjwa wa saratani.

 

By Warda Ahmed