HabariMombasa

Waziri Magoha azuru mitaa ya mabanda ya Jomvu na Changamwe……

Waziri wa elimu Pro George Magoha  leo anafanya ziara katika mitaa ya mabanda eneo la Jomvu na Changamwe kuwatembelea wanafunzi ambao watanufaika na msaada wa elimu kutoka kwa mpango wa ufadhili wa elimu.

Wanafunzi 9,000 kote nchini watanufaika na mpango huo, 62 wakitoka katika mtaa wa Bangladesh hapa Mombasa.

Aidha Magoha amesema kuwa wanafunzi wote watakaonufaika na mpango huo wa serikali watapelekwa katika  shule za mabweni ili kuwapa wakati mwema wa kujiendeleza kimasomo.

 

By Reporter