HabariMombasa

KPA kuandaa uchaguzi wa wafanyikazi hapo kesho….

Uchaguzi wa wafanyikazi katika halmashauri ya bandari nchini KPA unatarajiwa kufanyika hapo kesho kote nchini,lakini utata umeibuka baada ya baadhi ya wagombeaji kuelekea katika mahakama ya Mombasa kusimamisha shughuli hiyo.

Wagombeaji hao wanataka bodi ya uchaguzi ifutiliwe mbali kwa madai kwamba ilichaguliwa kisri na baadhi ya wagombeaji.

Aidha wanadai kwamba hakuna kikao kilichoitishwa na bodi hiyo, kukutana na wagombeaji wote ili kuzungumzia mikakati na utaratibu ulioweka kuhakikisha shughuli hiyo itakuwa huru.

Hatahivyo baadhi ya wagombeaji wameitetea bodi hiyo ya uchaguzi.

By Warda Ahmed