BurudaniEntertainmentHabari

KFCB yateua mabalozi wa kusambaza ujumbe wa maadili mema kuhusu sanaa…..

Bodi ya kutathmini ubora wa filamu nchini KFCB imewataka wakenya kutilia mkazo maadili hasa katika Sanaa huku ikiwateua mabalozi wa kusambaza ujumbe huo katika jamii.

Mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua ameyataka mashirika husiika hususan ya kiserikali kushirikiana na jamii, wazazi na vyombo vya habari ili kukuza maadili mema katika jamii.

Mutua amesema kwamba tatizo linaloikumba taifa la Kenya ni kupungua kwa maadili yetu akishikilia kwamba iwapo maadili mema yatakuzwa katika jamii basi patakuwepo na hisia za yaliyomema na yasiyomema

Kulingana na Margaret Gachagua ambaye ameteuliwa kuwa balozi wa bodi ya Kutathmini filamu KFCB amewataka viongozi kuwa makini wakti wawanapozungumza na wananchi kwani wao ni mifano ya kuigwa na vijana wengi.

By Joyce Kelly