HabariNewsSiasa

Mbunge wa Magarini Michael Kingi amesema ukanda wa Pwani utakuwa na chama chake katika uchaguzi wa mwaka wa 2022…

Mbunge wa Magarini Michael Kingi amesema ukanda wa Pwani utakuwa na chama chake katika uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Akizungumza katika eneo bunge lake Kingi amesema kwa muda sasa viongozi kaunti hiyo wamekuwa wakishiriki mazungumzo katika jihudi za kuimarisha mpango huo.

Amewataja baadhi ya viongozi eneo hilo kuwa wabinafsi hatua anayosema kucheleweshwa kwa chama hicho.

Wakati uohuo mbunge huyo ameapa kukihama chama cha chungwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa manufaa ya chama cha pwani.

Amewataka viongozi kuungana ili kutoa muelekeo mwafaka kwa wakazi ambao anadai wamechoshwa na vyama visivyokuwa vya eneo hilo.

Matamshi ya Kingi yanajiri huku Gavana wa kaunti hiyo Amason Kingi anayepigia upato chama cha pwani akisema anakumbwa na changamoto katika kutimiza hilo.

BY NEWS DESK