HabariMombasaNewsSiasa

Mbunge wa Msambweni kaunti ya Kwale Feisal Bader amepinga vikali kigezo cha kuwataka wabunge na wawakilishi wadi kuwa na cheti cha shahada.

Mbunge wa Msambweni kaunti ya Kwale Feisal Bader amepinga vikali kigezo cha kuwataka wabunge na wawakilishi wadi kuwa na cheti cha shahada.

Akizungumza huko Diani, Bader amesema kuwa kigezo hicho kinakiuka katiba ya nchi inayowaruhusu viongozi kuwania nafasi za serikali bila vikwazo vyovyote.

Mbunge huyo ameeleza kwamba hatua hiyo itawafungia nje viongozi wengi kutokana na idadi ndogo ya wakenya waliopata cheti cha shahada.

Aidha, Bader ameahidi kuwa bunge la kitaifa litaifanyia marekebisho mswada huo unaofaa kuanza kutekelezwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kwa sasa, rais na naibu wake pamoja na magavana na manaibu wao ndio wanaopaswa kuwa na shahada.

BY NEWS DESK