HabariSiasa

Ruto asisitiza kwamba marekebisho ya katiba lazima yamzingatie mwananchi………

Naibu rais William Ruto ameshikilia kauli yake kwamba

mpango wa kufanyia marekebisho katiba lazima uzingatie kuboresha maisha ya wananchi wa chini.

 

Akizungumza huko Nakuru, Ruto amesema ni jambo la kusikitisha kuona viongozi wachache serikalini kujihusisha na kufanyia marekebisho sheria za ardhi nchini kwa maslahi yao wenyewe.

 

Wakati huo huo Ruto, amesuta vikali mipango ya kutaka kuunganisha chama cha Jubilee na ODM kwa lengo la kuteua atakayepeperusha bendera ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

 

Ruto alikuwa ameandamana na gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui, na wabunge wakiwemo Aisha jumwa wa Malindi.

By Warda Ahmed