Habari

DHAHABU GHUSHI YAPATIKANA KATIKA UWANJA WA NDEGE JKIA

 

Maafisa wa idara ya upelelezi na jinai DCI wamepata dhahabu ghushi iliyokuwa imehifadhiwa katika  kituo cha ndege kuelekea nchini Uswizi katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na maafisa hao mtandao wa  walaghai wa biashara hiyo ya dhahabu umegunduliwa na unawahusisha maafisa wakuu serikalini.

Dhahabu hiyo ghushi iliyopakiwa katika makasha 31 iliingizwa nchini kutoka taifa jirani la Uganda.

Inaaminika kuwa wafanyibiashara walaghai huziifadhi dhahabu zenyewe katika uwanja huo wakidai ni mizigo inayosubiri kusafirishwa kuelekea mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Kulingana na polisi imegunduliwa kwamba baadhi ya wahusika wa biashara hiyo wamejinunulia mali ya mamiloni ya pesa katika mitaa ya kifahari humu nchini.

Aidha wahusika hao vilevile wanahusishwa na sakata ya mwaka 2019 ambapo bidhaa ghushi zilipatikana katika benki mbalimbali nchini.

BY JOYCE MWENDWA