HabariMichezo

MASHINDANO YA SAFARI RALLY KUFANYIKA NCHINI HADI 2026

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa mashindano ya magari ya langalanga maarufu kama Safari Rally yatakuwa yanafanyika nchini kila mwaka hadi mwaka wa 2026.

Akizungumza kwenye hafla ya kumalizika kwa mashindano hayo rais Kenyatta amesema uamuzi huu umeafikiwa baada ya mazungumzo na bodi inayoongoza ya mchezo wa magari FIA na

WRC

Bingwa wa dunia Sebastian Ogier ameibuka mshindi sekunde nane mbele ya Takamoto Katusta wa Japan aliyemaliza wa pili.

Dereva Thierry Neuville kutoka Ubelgiji ambaye alikuwa akiongoza mashindano hayo katika siku ya pili alijiondoa hii leo baada ya gari lake kugonga mwamba.

 

BY JOYCE MWENDWA