HabariMazingira

TAHARUKI YATANDA KATIKA MAENEO YA KON NA GOTU KATIKA MPAKA WA ISIOLO NA SAMBURU

Taharuki imetanda katika maeneo ya Kon na Gotu katika mpaka wa Isiolo na Samburu kufuatia mapigano ambayo yalianza siku ya Ijumaa na kuendelea hadi hapo jana na kusababisha watu wanne kujeruhiwa kwa kupigwa risasi

Inaarifiwa kuwa mapigano hayo ni baina ya wafugaji katika kaunti hizo mbili

Kulingana na wakaazi wafugaji hao walihamia maeneo hayo kutafuta maji na malisho ya mifugo wao, kufuatia kipindi kirefu cha kiangazi kinachoendelewa kushuhudiwa kwenye kaunti za Samburu na Isiolo.

Maafisa wa usalama wanasema watu 50 wamefariki dunia tangu mwezi Januari mwaka huu huku mwezi huu pekee 15 wakiuliwa

Viongozi wa kisiasa eneo hilo sasa wanamuomba waziri wa masuala ya ndani ya nchi dkt Fred Matiang’I kuingilia kati huku wakisema maafisa wa usalama kwenye maeneo hayo wanazembea

BY JOYCE MWENDWA