Habari

Msongamano wa wananchi kuwasilisha ushuru wa KRA washuhudiwa……

Msongamano mkubwa wa wananchi unaendelea kushuhudiwa katika vituo vya kuwasilisha ushuru wa mwaka 2020 kwa mamlaka ya KRA, yaani filing returs huku ikiwa imesalia siku moja tuu kwa makataa kukamilika.

Baada ya kutembelea vituo mbali mbali hapa Mombasa ikiwemo huduma centre na shemu baadhi ya Cyber Café ikwemo afisi ya halmashuari ya KRA, wananchi walikuwa wemejaa pomoni kukimbilia dakika za mwisho kama kawaida yao, za kuwasilisha ushuru huo.

Baadhi ya wananchi tuliozungumza nao walikuwa na haya ya kusema.

Ikumbukwe kwamba zoezi la kuwasilisha ushuru wa kila mwaka hutamatika tarehe 30 ya mwezi juni n na iwapo mwananchi yeyote mwenye nambari ya pin ya KRA atakuwa hajawasilisha uhuru huo basi hutozwa faini ya shilingi elfu 2.

 

By Allan Preston