Habari

Wizara ya usalama yahimizwa kukabiliana na utekaji nyara….

 

Wizara ya usalama nchini imehimizwa kukabiliana na ongezeko la visa vya utekaji nyara ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa siku za hivi karibuni hususan maeneo ya ukanda wa pwani.

Kulingana na mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za binadamu mjini Kilifi, KIlifi Mums, Kibibi Ali ni kuwa hali inayoendelea kushuhudiwa imesababisha wasiwasi kwa wananchi.
Amewataka wazazi kuwa waangalifu zaidi na watoto wao ili kuepuka visa kama hivi hususan wakati wanapocheza na wakati wakiwa shuleni.

Ali ametoa wito kwa wazazi kukoma kuandika majina ya watoto wao kwenye mikoba yao ya shule pamoja na barakoa zao ili kuepuka watekaji nyara kupata fursa ya kuyajua majina ya watoto na kufanya utekaji nyara kwa watotokuwa rahisi.

 

By Kilifi correspondent