Habari

SERIKALI YA KITAIFA KUPITIA IDARA YA ELIMU YAANZA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA WANAKABILIANA NA JANGA LA CORONA KATIKA SHULE KAUNTI YA KILIFI

Serikali ya kitaifa kupitia kwa idara ya Elimu kwa ushirikiano na wadau mbalimblai nchini imeanza mikakati ya kuhakikisha wanakabiliana na janga la Corona katika shule zilizoko kaunti ya Kilifi.

Wadau waliohusishwa ni maafisa wa shirika la AMREF na Benki ya ABSA nchini, ambao wamejitosa katika vita dhidi ya Corona katika shule kwa kutoa vifaa vya kukinga Corona mbali na kujenga sehemu za kuosha mikono zitakazotumiwa na wanafunzi pamoja na waalimu shuleni

Andrew Mchange ambaye ni mkurugenzi katika shirika la AMREF nchini amesema ipo haja ya kila mmoja kuhakikisha kuwa Corona inaepukwa kwa kuziba mianya yote ya kuendeleza msambao.

Kauli yake imeungwa mkono na mkurugenzi wa benki ya ABSA ukanda wa pwani James Agin ambaye amesisitiza jukumu la kuhakikisha afya njema miongoni mwa wanafunzi hasa wakti huu wa Corona si wa serikali pekee bali ni wa kila mmoja wetu.

 

BY JOYCE KELLY MWENDWA