Habari

Mahakama kuu Mjini Malindi yamuamuru Inspekta Wa Polisi Hillary Mutyambai kumuawasilisha Dereva Yassir Hemed

Mahakama kuu mjini Malindi imemuamrisha inspekta wa polisi Hillary Mutyambai kumwasilisha dereva wa ambyulensi Yassir Hemed ambaye alitoweka baada ya kutishiwa na polisi na tarehe 19 mwezi uliopita.

Jaji wa mahakama ya malindi Reuben Nyakundi,amesema  haki za Hemedi zilikiukwa kwa kutishiwa na maafisa hao na kisha kuripotiwa kutoweka.

Uamuzi huu unajiri kufuatia rufaa iliyowasilishwa na shirika la kutetea haki za kibindamu MUHURI kuitaka idara ya polisi kumuwasilisha mahakamni iwe yu hai au amefariki.

Jaji Nyakundi amesema kwamba amelitaja ombi na uamuzi huo kuwa la dharura na kuzitaka pande zote husika kumkabidhia stakabadhi za agizo lake mara moja.

Wanaohusika katika kesi hiyo ni afisi ya murugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, Inspekta mlkuu wa polisi, kamanda wa polisi wa Lamu na mwenziwe wa mpeketeni vilevile idara ya upelelezi DCI kaunti ya Lamu.

Hemedi alitekwa nyara tarehe 19 mwezi ulopita katika eneo la mkunumbi kaunti ya Lamu

BY CAROLINE