HabariSiasa

MAHAKAMA YA RUFA A YASTISHA KUAPISHWA KWA ANNE KANANU

Mkanganyiko wa uhali wa kuhudumu kwa naibu gavana wa Nairobi Anne kananu umejitokeza tena hii leo baada ya mahakama ya rufaa kusitisha shughuli ya kuapishwa kwake kufuatia rufaa iliyowasilishwa na mwanaharakati Okiya Omtatah.

Majaji wa mahakama ya rufaa Jessie Lessit, Wanjiru Karanja na Jamilla Mohammed waliokuwa wakiskiza rufaa hiyo wamesema agizo la kuzuia kwa kuapishwa kwa Kananu litaendelea kutekelezwa hadi Oktoba tarehe 22 ambapo mahakama itatoa mwelekeo zaidi.

Ikumbukwe kuwa Kananu aliapishwa miezi kadhaa na hata kuanza kutekeleza majukumu yake katika wadhfa wa naibu gavana.

Hata hivyo Kananu ametangaza wazi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi mkuu ujao.

 

BY CAROLINE NYAKIO