HabariMazingira

USAFIRI WA BODABODA WATAJWA KAMA KERO KAUNTI YA LAMU

Shirika la Muhuri pamoja na washikadau wengine katika kaunti ya Lamu wameandaa kongamano pamoja na wakazi na wanabodaboda katika eneo la Fort ili kujadili usafiri wa bodaboda ambao umetajwa kuwa kero kwa wakazi wa kaunti hiyo.

Kulingana na afisa wa shirika hilo ni kwamba ongezeko la bodaboda limechangia pakubwa kuwepo kwa ukosefu wa usalama akiwataka wakaazi wa Lamu kusimama kidete katika kufanya uamuzi mwafaka wa kuukomboa mji wao.

Wahudumu wa bodaboda wanalaumiwa kwa kujihusisha na uhalifu jambo ambalo wanadai limepunguza idadi ya watalii na vilevile kuchangia katika ongezeko la visa vya ajali kisiwani humo.

Washikadau aidha wametaka kutekelezwa kwa sheria za barabarani.

Vilevile waakazi wametaka kuondolewa kwa huduma za bodaboda mjini Lamu.

 

BY PRESTON WANDERA