AfyaHabari

SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA YAPEWA SAA 72 KUWALIPA WAFANYIKAZI WA AFYA

Serikali ya kaunti ya Mombasa imepewa saa 72 kuwalipa wafanyikazi wa afya katika kauti ya Mombasa la sivyo maafisa hao waelkee mgomoni.

Akizungumza na sauti ya pwani fm katibu mkuu wa maafisa wa kliniki KUCO tawi la Mombasa Franklin Makanga, amesema serikali ya kaunti iliwaahidi kuwalipa mishahara na marupurupu yao ila hadi wa sasa hakuna lililofanyika.

Maafisa hao wanalilia haki wakidai kuwa serikali ya kaunti hiyo inawaghadhabisa kwa kutowalipa mishahara yao hatua ambayo imewapelekea kuishi maisha magumu mno.

Mmoja wa maafisa hao  anayefanya kazi katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani coast General,ambaye majina yake tumeyabana, anasema kuwa serikali ya kaunti hiyo imekataa kuwalipa mishahara tangu waliporudi kazini kutoka mgomo uliochukua muda wa miezi 3.

 

BY DAVID OTIENO