HabariNewsSiasa

JUBILEE BADO NI IMARA ASEMA KIMUNYA…

Kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Amos Kimunya amesema kwamba chama cha Jubilee kiko imara na hakijasambaratika kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozi nchini

Akizungumza mjini Mombasa Kimunya amekashifu viongozi wanaoeneza propaganda kwamba chama hicho kimepoteza umaarufu wake.

Hata hivyo ametaja haja ya viongozi wa chama hicho kuungana na kuimarisha mikakati yake ili kiweze kuwa imara hasa wanapojitayarisha kwa uchaguzi wa mwaka 2022.

BY ALLAN WANDERA