KimataifaNews

WINGS TO FLY YAFADHILI WANAFUMZI 10,705…

Wanafunzi 10,705 kutoka familia zisizojiweza kote nchini wamepokea ufadhili kutoka Benki ya Equity chini ya mpango wa wings to fly ili kuwawezesha kujiunga na kidato cha kwanza jumatatu juma lijalo.

Akizungumza kwenye hafla ilioandaliwa katika Shule ya upili ya Ngahu iliyopo Mjini Nanyuki, Afisa Mtendaji Mkuu wa banki ya Equity daktari James Mwangi amesema ufadhili huo wa masomo utahudumia ada ya masomo, malazi, usafiri na fedha za matumizi.

Zaidi ya wanafunzi 114,000 walituma maombi ya kusijali kwenye mpango huo huku Mwangi akiishukuru serikali ya kenya kwa kuanzisha mpango wa elimu ya sekondari bila malipo ili kuwawezesha wale ambao hawajafanikiwa maishani kutimiza ndoto zao.

BY NICKY WAITA