Habari

KARO YAPUNGUZWA KATIKA SHULE ZA UPILI

Waziri wa elimu George Magoha ametangaza kupunguzwa kwa karo katika shule za upili kote nchini kutokana na ufupi  wa kalenda ya shule ya mwaka huu.Shule za kitaifa wanafunzi wanatakiwa kulipa shilingi 45,054 huku zile  za kaunti zinatakiwa kulipa 39,554 ambapo shule za kitaifa zimepunguziwa jumla ya shilingi 8,500 huku zile za kaunti zikipunguziwa shilingi 5,500.Waziri Magoha ameyazungumza haya hii leo katika hafla ya kuzindua  ufadhili wa elimu kwa wanafunzi zaidi ya 9,000 waliofanya mtihani kwa kitaifa wa KCPE mwaka huu  kutoka katika maeneo yaliotengwa ili kufadhili masomo yao ya sekondari.Aidha katibu katika wizara ya elimu nchini Julius Jwan ametoa wito kwa wazazi wote kulipa karo kwa wakati unaofaa ili kuendeleza shuhuli za masomo katika taasisi za elimu huku akisema kuwa masomo yataendelea huku kanuni za masharti ya kudhibiti msambao wa virusi vya korona yakizingatiwa kwa kina.

 

By News Desk