Habari

MABADILIKO YA CHUO KIKUU CHA NAIROBI YASITISHWA

Mahakama ya uajiri na Leba imesitisha kwa muda kutekelezwa kwa mabadiliko katika chuo kikuu cha Nairobi hadi pale kesi iliyowasilishwa mahakamani kusikilizwa na kuamuliwa.

Chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu nchini WASU kiliwasilisha kesi mahakamani kupinga mabadiliko hayo yaliotangazwa mnamo julai 14.

Kupitia wakili wa chama hicho Titus Koseo, wasu inasema kwamba mabadiliko hayo yalikiuka katiba kwani wahusika wote hawakuhusishwa.

Uamuzi huu unajiri siku tatu pekee baada ya waziri wa elimu profesa George Magoha kuagiza mabadiliko hayo yasitekelezwe.

Chuo kikuu cha Nairobi kiliondoa nafasi tano za manaibu wakuu na badala yake kubuni nafasi mbili pekee za wasaidizi wa mkuu wa chuo hicho.

 

BY REPORTER