AfyaHabari

Serikali ya Kwale kuendeleza hamasa za chanjo ya Kuzuia saratani ya kizazi……………

Serikali ya kaunti ya Kwale inaendezeza hamasa dhidi ya umuhimu wa kupokea chanjo ya kuzuia saratani ya kizazi miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka kumi.

Kulingana na waziri wa afya katika kaunti hio Francis Gwama, zoezi hilo linalenga wasichana walioko shuleni na ambao wako katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huo.

Kwa upande wake mwakilishi wadi maalum katika bunge la Kwale Mishi Mayumbe amebaini kwamba vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano katika kaunti hio vimepungua kutokana na juhudi za serikali ya kaunti ya kwale za kuboresha hudma za afya.