HabariNews

Serikali yatoa Sh17 bilioni kwa shule za umma kwa mwaka wa masomo wa 2021…………………….

 

Waziri wa Elimu George Magoha alisema Serikali ilitoa Sh17.47 bilioni kama ufadhili wa jumla kwa wanafunzi wote.

Kati ya hizi, Sh2.62 bilioni zinalenga wanafunzi wa shule za msingi wakati Sh14.85 bilioni ni kusaidia wanafunzi wa shule za sekondari.

Magoha alisema ada yoyote ya nyongeza nje ya mwongozo rasmi haitavumiliwa.

Alisema Serikali inavutiwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza ambao walianza kuripoti katika shule zao za upili Jumatatu, Agosti 2, 2021.

Zaidi ya wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, wanafunzi wengine wote walifanikiwa kufungua kwa Muhula wa Kwanza wa kalenda ya masomo ya 2021 mnamo Julai 26, 2021.

Huku hayo yakijiri Serikali zote za kaunti nchini zinatarajiwa kupata shilingi milioni kumi kila moja kutoka kwa serikali kuu.

Katibu mkuu katika wizara ya elimu nchini Dkt Mwakima anaesema fedha hizo zitasaidi kuwezesha na kufufua vyuo vya kiufundi katika kaunti hizo.

Hapo awali serikaliza kaunti zilikuwa zikipewa bilioni mbili kugawanya kwa kila kaunti.