HabariNews

Serikai ya Kaunti ya Tana River yatangaza kuwachukulia hatua Madereva wa Ambulansi wanaosababisha ajali……………….

Serikali ya kaunti ya Tana River imetangaza kuwachukulia hatua za kinidhamu madereva wa ambulensi wanaosababisha ajali.

Gavana wa kaunti hiyo Mejja mustafu Dhadho Godhana amesema magari mengi ya wagonjwa mahututi yameharibika kwa sababu uendeshaji ovyo wa madereva hao.

Gavana huyo ameleza kuwa kaunti hiyo kufikia sasa iko na ambulensi 18 ambapo 12 pekee kati ya ambulensi hizo ndizo zilizo katika hali shwari.

Gavana huyo ameeleza kuwa kuharibika kwa magari hayo kunasababishwa na kuajiriwa kwa madereva wasiokuwa wazoefu.