HabariMichezoNews

Nicholus Kimeli mbioni Kushinda dhahabu katika mbio za mita elfu tano………………..

Nicholas Kimeli ameelezea matumaini ya kushindia kenya nishani ya dhahabu katika mbio za mita 5000 siku ya ijumaa.

Hii ni baada ya kutumia dakika 13 sekunde 38 nukta nane saba kutwaa ubingwa kwenye semi fainali.

Wakenya wengine kwenye mbio hizi Daniel Simiyu na Samuel Chebole wameshindwa kufuzu kutokana na sababu tofauti.

Kwenye mbio za mita 400 kina dada muakilishi pekee wa kenya Hellen Syombua ameshindwa kuendelea na michezo hii baada ya kumaliza katika nafasi ya tano.

Ratba kamili ya mashindano hayo siku ya Jumatano  Agosti 4 ni kama ifuatavyo.

1pm…semi fainali mbio za mita 1500 kina dada.

2pm…mita 3000 steeplechase kina dada fainali.

3.05pm…mita 800 fainali wanaume.