AfyaHabari

KMPDU yaitaka serikali kuajiri madaktari zaidi….

Katibu mkuu wa Chama cha madaktari nchini KMPDU Davji Atellah ametoa wito kwa serikali kuu kuajiri madaktari.

Atellah amesema hatua hii imetokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona humu nchini.

Haya yanajiri huku baadhi za kaunti zikiweka masharti ya kukabiliana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Kaunti ya Mombasa imeweka masharti kadhaa ikiwa ni pamoja na kusitisha mikutano yote ya umma, Maabadi kuwa na thuluthi moja ya waumini, Chanjo ya Corona kutolewa kwa wote pamoja na kusitishwa kwa tamasha ndani ya vilabu na hoteli.

Hatua hii ikijiri siku moja baada ya kaunti ya Kwale kusitisha shughuli zote za michezo.

Hapo jana wizara ya afya ilitangaza visa 1,085 vipya vya maambukizi ya Corona huku asilimia ya maambukizi ikiwa 15.4.

 

By Joyce Mwendwa