HabariSiasa

Rais Uhuru Kenyatta Awateuwa makamishna wa IEBC…………….

Rais Uhuru Kenyatta amewateua Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Cherop,na  Justus Abonyo kuwa makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Wanne hao sasa watarudishwa  katika kamati ya haki na masuala ya kisheria bungeni inayoongozwa na Mbunge wa Kangemi Muturi Kigano, kupigwa msasa kabla ya kutangazwa rasmi.

Makamishna hao wataziba pengo la aliyekuwa kamanishna Roselyn Akombe, Margaret Mwachanya, Paul Kurgat, na aliyekuwa naibu mwenyekiti Consolata Maina.

Spika wabunge la kitaifa Justin Muturi ameigiza kamati husika bungeni kufuatilia uteuzi huo na kuwasilisha  ripoti chini ya siku 28.

 

By News Desk