HabariTravel

Magari Ya Ummah sasa kubeba abiria asilimia mia moja ………….

Ni afueni kwa wafanyikazi katika sekta ya uchukuzi baada ya serikali kupitia wizara ya uchukuzi kuruhusu magari ya umma kubeba asilimia 100 ya abiria kama inavyotakiwa.

Haya yanajiri baada ya sekta hiyo kukadiria hasara kubwa kutokana na ujio wa virusi vya korona uliolazimu serikali kuweka mikakati ya kudhibiti msambao wa virus hivyo kwa kuyataka magari ya umma kubeba asilimia 60 ya abiria.

Akizungumza na vyombo vya habari katibu wa utawala katika wizara hiyo Chris Obure amesema kwamba zoezi hilo litaaza rasmi Jumatatu 9 Augosti mwaka huu   akionya kuwa   mashirika ya matatu maarufu (SACCOS) ambayo yataenda kinyume na masharti ya wizara hiyo yatapokonywa leseni zao.

Aidha katibu huyo ametoa wito kwa wakenya wote kuhakikisha kuwa wamechukua jukumu la kujilinda wao wenyewe kutokana na maradhi hayo hatari na pia wenye magari kuzingatia sheria za kudhibiti msambao huo.