AfyaHabari

Wenye akili taahira wapokea chanjo ya Astrazeneca hapa Mombasa…………..

Zaidi ya watu 60 wenye akili taahira wamepata chanjo dhidi ya virusi vya corona ya Astrazeneca katika makazi yao yaliyoko eneo la Miritini hapa mjini Mombasa.

Akiongea na wanahabari, mkurugenzi wa Mombasa Women Empowerment Amina Abdalla amesema hatua hiyo itachangia kukabili mkurupuko wa ugonjwa huo wa Corona ambao unadaiwa kuongezeka.Amina ameiomba serikali kuwapatia vitambulisho waathiriwa hao ili kurahisisha kuwafuatilia kwa awamu ya pili ya chanjo hiyo.

BY JAPHETH MAKANAKI