HabariNewsSiasa

JAMES ORENGO AMTAKA RUTO KUFIKA MBELE YA KAMATI YA BUNGE LA KITAIFA …

Seneta wa kaunti ya Siaya James Orengo ametoa malalalimishi yake kuhusiana na uhusiano baina ya naibu wa rais dkt William Ruto na mshirika wake wa uturuki Harun Aydin akitaka Ruto kufikishwa mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kueleza kinagaubaga uhusiano huo.

Akizungumza na wanahabari, Orengo amedokeza kuwa angetaka naibu wa rais William Ruto kuhojiwa na wabunge katika bunge la kitaifa ili aeleze kina cha mikutano yake na mturuki huyo akidai kuwa biashara za Aydin si za kuaminika.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya waziri wa usalama wa ndani dkt Fred Matiangi kusema kuwa serikali ilimfurusha Harun Aydin kwa kuhusika na biashara ya pesa haramu na kwamba Kenya haikuomba msahama kuhusu hatua hiyo kama alivyotaja naibu wa rais William  Ruto.

Matiangi alikuwa akihojiwa na kamati ya bunge kusuhu usalama mjini Mombasa.

BY CAROLINE NYAKIO.