HabariNews

Watahiniwa wa KCSE mwaka 2020 kujua vyuo vikuu ambavyo watajiunga navyo leo…..

Watahiniwa wa mtihani wa KCSE mwaka 2020 wanatarajiwa kujua vyuo vikuu ambavyo wamechaguliwa kujiunga navyo hiii leo.

Waziri wa elimu proffesa George Magoha anatarajiwa kutangaza orodha hiyo.

Jumla ya watahiniwa 747, 161 walifanya mtihani huo mwaka huu huku wanafunzi 143,140 wakifikisha alama ya C+  inayohitajika ili kuhitimu kuingia chuo kikuu kwa ufadhili wa serikali.

Idadi hiyo imeongezeka kwani mwaka wa 2019 ni wanafunzi 125,746 pekee ambao walihitimu.

Mnamo Ijumaa mkurugenzi mkuu wa KUCCPS alisema kuwa waziri George Magoha angetoa maelezo zaidi hadharani kuhusu hatua hiyo.

Mwaka uliopita vyuo vikuu vya umma vilichukua watahiniwa 108,378 ambao walikalia mtihani mwaka wa 2019 huku 17,368 wakichukuliwa katika vyuo vikuu vya kibinafsi.

BY  NEWS DESK.