HabariMombasaNewsSiasa

Viongozi wa ODM Mombasa waanza kuimarisha chama hicho mashinani……..

Akizungumza kwenye zoezi la usajili katika Wadi ya Tudor hapa Mombasa ambapo Zaidi ya wanawake 200 wamejisajili kujiunga na chama hicho,mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji katika bunge la kitaifa aliyepia mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir,amewaelezea wakaazi kuwa chama hicho cha ODM ni chenye kuwajali wanyonge kinyume na dhana ya baadhi ya viongozi wapinzani.

Ameyasema haya kufuatia wito kutoka kwa  kinara wa chama cha ODM Raila Odinga kuwataka wajumbe wa chama hicho katika bunge la kitaifa kuwasilisha mswada bungeni ili kutetea hali ya uchumi nchini pamoja na kupendekeza suala la chanjo kwa wote.

Hata hivyo amewahimiza wakaazi wa hapa Mombasa kuchanjwa akisema huenda serikali ikapata sababu ya kutofungua uchumi endapo wananchi hawatajitokeza kuchanjwa.

By Reporter