HabariNewsSiasa

Raila asema atakubali uamuzi wowote wa mahakama kuhusu BBI…..

Kinara wa ODM Raila odinga amesema hatakata rufaa dhidi ya uamuzi wa BBI unaotarajiwa siku ya ijumaa iwapo uamuzi huo hautamridhisha.

Raila amesema kwa sasa anaagazia zaidi mipango ya uchaguzi mkuu unaokuja.

Hapo jana Raila alikariri utayari wake kuheshimu maamuzi ya mahakama na kuashiria kwamba huenda ukawa mwisho wa BBI iwapo uamuzi huo utakuwa tofauti na matarajio.

Ikumbukwe kwamba awali aliwahi kutaja kuwa na mpango mbadala iwapo BBI itasitishwa na mahakama.

BY NEWS DESK