AfyaHabariNews

Serikali kupokea chanjo zaidi za Johson&Johson na Moderna…….

Serikali inatarajia kupokea chanjo zaidi aina ya Pfizer Johnson & Johnson na Moderna baada ya kupokea usaidizi wa  chanjo  elfu 407 za Astrazeneca kutoka taifa la Uingereza kupitia mpango wa COVAX.

Akizungumza wakati wa kupokeachanjo hizo, mkurugenzi wa matibabu dkt Patrick Amoth, amesema Kenya itapokea chanjo milioni 1.7 aina ya Moderna, chanjo elfu 393 za Johnson$Johnson na milioni 1.8 za Pfizer.

Usaidizi huu wa chanjo utasaidia serikali katika kufikia malengo ya kuchanja watu milioni 10 ifikapo mwisho wa mwaka huu .

Amoth amewaomba wananchi kujitokeza ili kupokea chanjo katika vita dhidi ya corona ili kuwezesha hali ya kawaida kuregea nchini .

Kufikia sasa zaidi ya watu milioni 2 wamepata dozi ya kwanza ya  chanjo ya astrazeneca  huku watu milioni 1.3 wamepata dozi ya pili.

BY NEWS DESK