Habari

Washukiwa wawili wa ugaidi wakamatwa katika kivuko cha Ferry Likoni………………

Maafisa wa polisi wamefanikiwa kuwakamata washukiwa wawili wakigaidi wakiwa na silaha hatari katika kivuko cha Likoni Ferry mapema leo.

Maafisa hao walifanikiwa kuwanasa magaidi hao waliokuwa katika gari dogo aina ya Probox yenye nambari ya usajili ya KCE 695 U, wakisubiria ferry kuvuka kuelekea eneo la kisiwani.

Polisi wamefanikiwa kuwapata na bunduki za aina ya AK47, vilipuzi na simu kadhaa.

Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa wakati wa tukio hilo.

Hata hivyo baadhi ya wananchi hapa Mombasa wanasema kwamba oparesheni hiyo ni ya uzushi tuu ili kuwadanganya wananchi wa Mombasa kwani wananchi wengi wamekuwa wakipotea huku wengi wao wakidaiwa kutekwa na maafisa kutoka kitengo cha ATPU.

Baadhi ya wananchi mitandaoni wamezua hisia mseto wakishangazwa vipi wanahabari walifika eneo hilo la tukio wakati tukio hilo likitokea ikiwemo kukamatwa kwa washukiwa hao.