Habari

Waziri Magoha aanzisha oparesheni Kuhakikisha wanafunzi wote wanajiunga na shule za Upili?

Waziri wa elimu Prof. George Magoha ameanzisha oparasheni ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliomaliza darasa la 8 wanajiunga na shule za upili.

Waziri Magoha ambaye amezuru mitaa ya mabanda ya Bangladesh na Kibarani katika kaunti hii ya Mombasa ameesema kuwa aslimia 40 ya wanafunzi bado hawajajiunga na shule za upili.

Kulingana na waziri huyo kaunti ya Mombasa ni miongoni mwa kaunti ambayo ina idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajajiunga na shule za upili pamoja na kaunti za Kwale na Kilifi.

Magoha ameshinikiza haja ya kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata elimu ya sekondari huku wazazi wengi wakidai kuwa kukosa kufika shuleni kwa baadhi ya wanafunzi kunatokana na athari za tandavu ya korona kwa uchumi.

By Warda Ahmed