HabariNews

MUUNGANO WA UASU WASITISHA MGOMO…………

Muungano wa vyuo vikuu nchini UASU umesitisha mgomo ulioratibiwa kuanza rasmi hii leo baada ya makataa ya siku saba yaliyotolewa na katibu mkuu wa chama hicho kutamatika.

Akizungumza na wanahabari, katibu mkuu wa UASU Constatine Wasonga amesema kuwa wamefutilia mbali mgomo wao ili waweze kuwa na mazungumzo zaidi na serikali kihusiana na malipo yao.

Wanachama wa UASU walifanya mkutano na katibu wa kudumu wa masomo ya vyuo vikuu na utafiti Simon Nabukwesi jijini Nairobi ambapo walijadili jinsi wizara la leba itasaidia kusuluhisha tatizo hili.

Wakati wa mkutano huo wahusika walikubalina kutathmini matokeo ya mazungumzo baina ya UASU na baraza la ushauri wa vyuo vikuu IPUCCF kuhusu kuchelewa kutekelezwa kwa mkataba huo wa maelewano wa CBA wa mwaka 2017 – 2021.

Iwapo mgomo huo ungefanyika hii leo ungeathiri masomo ya vyuo vikuu 35 nchini.

By News Desk